Sauti Juu Ya Maji Tafsiri ya Kiswahili
Sauti Juu Ya Maji Tafsiri ya Kiswahili
Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye
kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi
cha Mungu na cha Mwana – Kondoo
Ufunuo 22:1
Kupitia kote katika Neno la Mungu lililoandikwa,maji
yanaonekana sana yakielezea ukweli mkuu wa kiroho: uzima
wa milele wa Mungu unatiririka kutoka penye kiti chake cha
enzi kwenda kwa watu wake. Uzima wa yule ambaye
amekuwepo siku zote, na atakuwepo siku zote anaendelea
kuwapa uzima wale wanayoyaonea kiu maji haya, na wale
wanaomjia ili kunywa.
...
